>>KOCHA SIMBA: KUSAINI MKATABA WA MIEZI 18
>>TAIFA STARS: SAMATTA & ULIMWENGU NDANI!!
BAADA
ya danadana ya Siku kadhaa, Kocha mpya wa Simba kutoka Ufaransa,
Patrick Leiwig, hatimae alitua Jijini Dar es Salaam jana na kupokewa na
Katibu Mkuu, Evodius Mtawala, pamoja na Mamia ya Washabiki wa Klabu
hiyo.
Leiwig, ambae aliwahi kuifundisha Asec
Mimosa ya Ivory Coast na pia Timu za Vijana za PSG ya Ufaransa, alisema
anafahamu mambo mengi ya Simba na amejitayarisha vyema kuisaidia Timu
hiyo katika Mashindano ya ndani na nje ya Tanzania.
Kocha huyo pia alisema amepewa Taarifa
na Uongozi wa Klabu kuhusu safari yao ya kwenda Nchini Oman
kujitayarisha na Raundi ya Pili ya Ligi Kuu Vodacom inayoanza Januari 26
pamoja na Mashindano ya CAF.
Akiongelea kuhusu Kocha huyo, Katibu
Mkuu Mtawala amesema Kocha huyo atasaini Mkataba wa Miezi 18 na leo
anatarajiwa kusafiri na Kikosi cha Simba kwenda Zanzibar kwa ajili ya
Michuano ya Mapinduzi Cup inayoanza Januari 2.
+++++++++++++
MAPINDUZI CUP:
MAKUNDI:
KUNDI A:
Simba (Dar-es-Salaam),
Tusker (Kenya)
Bandari (Unguja)
Jamhuri (Pemba).
KUNDI B:
Azam FC (Dar-es-Salaam)
Mtibwa Sugar (Morogoro)
Coastal Union (Tanga)
Miembeni (Unguja).
+++++++++++++
Akiwa
Simba, Kocha Leiwig atasaidiwa na Moses Basena kama Mkurugenzi wa Ufundi
na Jamhuri Kiwele ‘Julio’ ambae ni Meneja wa Timu.
TAARIFA TOKA TFF:
Release No. 01
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Januari 1, 2013
WACHEZAJI 22 STARS WAITWA KAMBINI TAIFA STARS!!
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 22 watakaoingia
kambini Januari 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za
kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya
Morocco itakayochezwa Machi mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji hao
wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma saa 11.30 jioni
tayari kwa mazoezi yatakayoanza Januari 7 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa Juma
Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula na
Mwadini Ally wote kutoka Azam. Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir
Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin
Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman
Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo
(Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam),
Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho
Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa
Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali
(Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa
(Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred
Chimela (Mtunza vifaa).
CAF YAMTUMA LIUNDA KUKAGUA VIWANJA ETHIOPIA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF) limemteua ofisa wake Leslie Liunda wa Tanzania kwenda Ethiopia
kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa
utoaji leseni kwa klabu zitakazoziwezesha kushiriki michuano
inayoandaliwa na Shirikisho hilo.
Ofisa huyo atawasili nchini Ethiopia
kesho (Januari 2 mwaka huu) ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo
Januari 6 mwakani na baadaye kupeleka ripoti yake CAF.
Utekelezaji wa kazi yake hiyo nchini
Ethiopia utahusisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirikisho la Mpira wa
Miguu la Ethiopia (EFF), Wizara ya Michezo ya nchi hiyo, viongozi wa
klabu na mameneja wa viwanja husika.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment