Saturday, December 29, 2012

MAN UNITED YAMALIZA 2012 POINTI 7 KILELENI LIGI KUU ENGLAND!!

BPL_LOGORATIBA/MATOKEO:
Jumamosi 29 Desemba 2012

Sunderland 1 Tottenham 2
Aston Villa 0 Wigan 3
Fulham 1 Swansea 2
Man United 2 West Brom 0
Norwich 3 Man City 4
Reading 1 West Ham 0
Stoke 3 Southampton 3


[SAA 2 na Nusu Usiku] 
Arsenal v Newcastle

MANCHESTER UNITED 2 WEST BROM 0
Manchester United watauanza Mwaka mpya 2013 wakiwa kileleni mwa Ligi Kuu England wakiwa Pointi 7 mbele baada ya kuifunga West Bromwich Albion Bao 2-0 Uwanjani Old Trafford.

Bao la kwanza la Man United ni la kujifunga mwenyewe Gareth McAuley akijaribu kuokoa krosi ya Ashley Young.

Bao la Pili kwa Man United lilifungwa katika Dakika ya 90 na Robin van Persie, alietokea Benchi Kipindi cha Pili kumbadili Shinji Kagawa aliekuwa akicheza Mechi yake ya kwanza tangu Oktoba kufuatia kuuguza Goti lake.

VIKOSI:

Man United: De Gea, Smalling, Vidic, Evans, Evra, Carrick, Cleverley, Valencia, Kagawa, Young, Welbeck

Akiba: Lindegaard, Ferdinand, Giggs, Hernandez, van Persie, Scholes, Buttner.

West Brom: Foster, Jones, McAuley, Tamas, Ridgewell, Thorne, Brunt, Rosenberg, Dorrans, Odemwingie, Long

Akiba: Myhill, Morrison, El Ghanassy, Jara Reyes, Lukaku, Dawson, Fortune.

Refa: Jon Moss

STOKE 3 SOUTHAMPTON 3 

Bao la Dakika ya 90 la Cameron Jerome limewapa Stoke City, waliokuwa wakicheza Mtu 10, sare ya Bao 3-3 na Southampton.

Southampton ndio walitangulia kufunga kwa Bao la Lambert lakini Stoke wakasawazisha kupitia Kenwyne Jones.

Southampton wakaenda mbele kwa Bao 3-1 kwa mabao ya Jay Rodriguez na lile la kujifunga mwenyewe Andy Wilkinson kisha Stoke wakafunga Bao la pili kupitia Matthew Upson wakati Stoke wakicheza Mtu 10 kufuatia Kiungo wao Steven Nzonzi kupewa Kadi Nyekundu.

Ndipo likaja Shuti la Mita 30 lililohakikisha Stoke City wakiendelea na Rekodi yao ya kutofungwa katika Mechi 17.

VIKOSI:

Stoke: Begovic, Shotton, Huth, Upson, Wilkinson, Kightly, Whelan, Nzonzi, Etherington, Walters, Jones

Akiba: Sorensen, Palacios, Owen, Adam, Whitehead, Crouch, Jerome.

Southampton: Kelvin Davis, Hooiveld, Yoshida, Fonte, Shaw, Puncheon, Schneiderlin, Cork, Rodriguez, Do Prado, Lambert

Akiba: Boruc, Steven Davis, Ramirez, Fox, Richardson, Mayuka, De Ridder.

Refa: Mark Clattenburg

READING 1 WEST HAM 0

Leo Reading wamepata ushindi wao wa pili Msimu huo kwa Bao la Dakika ya 5 la Pavel Pogrebnyak.

VIKOSI:

Reading: Federici, Gunter, Mariappa, Pearce, Harte, Leigertwood, Karacan, Kebe, Guthrie, McAnuff, Pogrebnyak

Akiba: Taylor, Le Fondre, Hunt, Morrison, Tabb, Robson-Kanu, Cummings.

West Ham: Jaaskelainen, Tomkins, Collins, Reid, O'Brien, Noble, O'Neil, Taylor, Nolan, Jarvis, Cole

Akiba: Spiegel, Collison, Maiga, Vaz Te, Demel, Diarra, Spence.

Refa: Michael Oliver

ASTON VILLA 0 WIGAN 3
Wigan Athletic leo wamejinasua toka zile Timu 3 za mkiani na kupanda hadi nafasi ya 16 wakiwa juu ya Aston Villa, Timu ambayo leo wameichapa 3-0, na kuwashusha  hadi nafasi ya 17.

Bao za Wigan zilifungwa na Ivan Ramis, Emmerson Boyce na Arouna Kone.

VIKOSI:

Aston Villa: Guzan, Herd, Clark, Lichaj, Lowton, Ireland, Holman, Bannan, Bennett, Weimann, Benteke

Akiba: Given, El Ahmadi, Albrighton, Westwood, Bowery, Stevens, Carruthers.

Wigan: Al Habsi, Ramis, Caldwell, Figueroa, Boyce, McCarthy, Jones, Beausejour, Kone, Di Santo, Maloney

Akiba: Pollitt, Gomez, McManaman, McArthur, Boselli, Stam, Golobart.

Refa: Kevin Friend

FULHAM 1 SWANSEA 2

Wakiwa kwao Craven Cottage, Fulham wamefungwa Bao 2-1 na Swansea City waliocheza bila ya Straika wao hatari Michu na huu ni ushindi wao wa kwanza katika Mechi 5 za Ligi.

Mabao ya Swansea yalifungwa na Graham na De Guzman na la Fulham lilipachikwa na Ruiz.

VIKOSI:

Fulham: Stockdale, Riether, Hangeland, Hughes, Briggs, Dejagah, Sidwell, Karagounis, Frei, Ruiz, Berbatov

Akiba: Etheridge, Kelly, Riise, Senderos, Baird, Richardson, Rodallega.

Swansea: Tremmel, Rangel, Williams, Monk, Tiendalli, de Guzman, Agustien, Dyer, Hernandez, Routledge, Graham
Akiba: Vorm, Bartley, Britton, Shechter, Moore, Ki, Davies.

Refa: Andre Marriner

NORWICH 3 MANCHESTER CITY 4

Wakicheza Mtu 10 Uwanjani Carrow Road kufuatia Kadi Nyekundu kwa Mchezaji wao Samir Nasri, Mabingwa watetezi Manchester City walisimama kidete na kuibuka washindi kwa Bao 4-3 dhidi ya Norwich City.

Man City walitangulia kwa Bao 2 mbele ndani ya Dakika 4 za kwanza mfungaji akiwa Edin Dzeko lakini Norwich wakapata Bao moja lililofungwa na Anthony Pilkington.

Licha ya kucheza Mtu 10 kufuatia kutolewa Nasri, City walipiga Bao la 3 kupitia Sergio Aguero na Russel Martin akaifungia Norwich Bao la pili na kuifanya Gemu iwe 3-2 lakini shuti la Dzeko liligonga mwamba na kumbabatiza Kipa Mark Bunn na kuipa City Bao la 4.

Bao la 3 kwa Norwich lilifungwa na Russell Martin.

VIKOSI:

Norwich: Bunn, Martin, Turner, Bassong, Garrido, Snodgrass, Tettey, Johnson, Pilkington, Hoolahan, Morison

Akiba: Rudd, Howson, Jackson, Elliott Bennett, Barnett, Ryan Bennett, Kane.

Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy, Toure, Barry, Aguero, Silva, Nasri, Dzeko

Akiba: Pantilimon, Lescott, Milner, Sinclair, Javi Garcia, Toure, Tevez.

Refa: Mike Jones

SUNDERLAND 1 TOTTENHAM 2

Tottenham leo wameshinda Mechi yao ya 6 kati ya 8 kwenye Ligi walipotoka nyuma kwa Bao la Nahodha wa Sunderland, John O’Shea, na kushinda Bao 2-1 kwa Bao za Carlos Cuellar kujifunga mwenyewe na Winga Aaron Lennon kupiga Bao la pili na la ushindi.

VIKOSI:

Sunderland: Mignolet, Gardner, O'Shea, Cuellar, Kilgallon, Johnson, Larsson, Colback, McClean, Sessegnon, Fletcher

Akiba: Westwood, Campbell, Wickham, McFadden, Vaughan, Ji, Bramble.

Tottenham: Lloris, Walker, Dawson, Caulker, Naughton, Lennon, Sandro, Dembele, Bale, Adebayor, Defoe

Akiba: Friedel, Dempsey, Vertonghen, Huddlestone, Parker, Sigurdsson, Livermore.

Refa: Martin Atkinson
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumapili 30 Desemba 2012

[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Chelsea
[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool

Jumanne 1 Januari 2013

SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham

[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United

[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal

Jumatano 2 Januari 2013

[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland

[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

No comments:

Post a Comment