Friday, December 21, 2012

UEFA CHAMPIONZ LIGI: BAADA ya DROO, NINI WAMESEMA!!

>>RATIBA KAMILI YATOKA!!
>>REAL v MAN UNITED ni FEBRUARI 13
>> FERGIE: ‘NDIO BIGI MECHI RAUNDI YA TIMU 16!!’
+++++++++++++++++++
RATIBA:
[Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku]
Jumanne 12  Februari 2013
Celtic v Juventus
Valencia v Paris St Germain
Jumatano 13  Februari 2013
Real Madrid v Manchester United
Shakhtar Donetsk v Borussia Dortmund
Jumanne 19  Februari 2013
Arsenal v Bayern Munich
FC Porto v Malaga
Jumatano 20  Februari 2013
Galatasaray v FC Schalke
AC Milan v Barcelona
Jumanne 5 Machi 2013
Borussia Dortmund v Shakhtar Donetsk
Man United v Real Madrid
Jumatano 6 Machi 2013
Juventus v Celtic
Paris St George v Valencia
Jumanne 12 Machi 2013
Barcelona v AC Milan
Schalke v Galatasaray
Jumatano 13 Machi 2013
Bayern Munich v Arsenal
Malaga v FC Porto
+++++++++++++++++++
FERGIE_n_MOURINHOMara baada ya kumalizika kwa Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI hapo jana huko Nyon, Uswisi, Wadau mbalimbali waliibuka kutoa maoni yao kuhusu Ratiba hiyo na Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, alisema pambano la Real Madrid na Manchester United ndio ‘mpambano’ wa Raundi hiyo.
Real Madrid na Manchester United hawajakutana kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI tangu Robo Fainali ya Mwaka 2003 ambayo Real walishinda kwa jumla ya Mabao 6-5 baada ya kushinda Mechi ya kwanza 3-1 huko Santiago Bernabeu na kufungwa 4-3 Uwanjani Old Trafford huku Ronaldo de Lima akipiga Hetitriki.
Mbali ya pambano kuwa zito, Mechi hii itakuwa na mvuto kwani Cristiano Ronaldo atarudi Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu aihame Man United na kwenda Real Madrid Juni 2009 kwa Dau la Pauni Milioni 80.
Mara ya mwisho kwa Sir Alex Ferguson kumvaa Jose Mourinho ilikuwa kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2009 wakati Man United ilipoibwaga Inter Milan kwenye Robo Fainali baada ya kutoka 0-0 na kuifunga 2-0 Old Trafford kwa Bao za Vidic na Ronaldo.
Ferguson amesema: “Ni nafasi nzuri kwa Mashabiki wetu kumuona Ronaldo tena na mimi kukutana na Jose-itabidi niagize Mvinyo safi!”
+++++++++++++++++++
Man United v Real Madrid
-1957: European Cup-Nusu Fainali: Real washinda 3-1Madrid, sare 2-2 na Real kushinda Jumla ya Bao 5-3
-1968: European Cup-Nusu Fainali: Man United washinda 1-0 Old Trafford, sare 3-3 ugenini na Man United washindi Jumla ya Bao 4-3
-2000: European Cup-Robo Fainali: Sare 0-0 huko Bernabeu, Man United wafungwa 3-2 nyumbani
-2003: European Cup-Robo Fainali: Real washinda 3-1 nyumbani, Man United washinda 4-3 nyumbani, Real wapita Jumla ya Mabao 6-5.
+++++++++++++++++++
YAFUATAYO ni NINI KILISEMWA KUTOKA KWA WADAU MBALIMBALI:
Real Madrid
Mkurugenzi wa Real Madrid, Emilio Butragueno, aliewahi kuwa Straika wao zamani:  "Tungependa kucheza na Man United baadae lakini hata wao hawakufurahia!"
Barcelona
Makamu wa Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu "AC Milan ni Klabu kubwa Ulaya, inaheshimika. Kwa sasa hawachezi vizuri lakini mpira hubadilika Siku hadi Siku."
Bayern Munich
Mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge "Tunaijua Arsenal vizuril. Tunaridhika na Droo hii lakini hatuwadharau!"
Paris St Germain
Mkurugenzi wa Soka, Leonardo: "Siku zote ni ngumu kusema ni Droo nzuri au siyo!"
Valencia
Mkurgenzi wa Valencia, Fernando Giner: "Kama tumefika hapa basi sisi ni moja ya Timu Bora 16 Ulaya!"

No comments:

Post a Comment