Friday, May 31, 2013

LUIS SUAREZ: 'NI WAKATI MUAFAKA KUONDOKA!'

SUAREZ_n_IVANOVICSTRAIKA wa Liverpool Luis Suarez amesema sasa ni wakati muafaka kwa yeye kuondoka lakini hajafanya uamuzi wowote kuhusu nini afanye baadae.
 
Suarez, Miaka 26, ambae kwa sasa yupo kwenye Adhabu ya kufungiwa Mechi 10 kwa kumng’ata Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic, amekiri ni vigumu kuikataa Real Madrid huku kukiwa na uvumi wa yeye kuunganishwa na kuhamia Klabu hiyo.

Amesema: “Ni wakati muafaka kubadilisha mazingira kwa sababu ya yale yaliyonitokea  huko England. ”

Suarez: 

-Goli 30 kwa Mechi 44 alizochezea Liverpool Msimu wa 2012/13 

-Tangu ajiunge Liverpool kutoka Ajax Januari 2011, amefunga Goli 51 katika Mechi 96. 

-Alifunga Bao 49 katika Mechi 48 alizochezea Ajax kabla kujiunga Liverpool 

-Amefunga Bao 31 kwa Mechi 62 alizochezea Uruguay 


Aliongeza: "Sijui wapi nitakwenda na sijui kama nitabaki!"

Suarez, ambae pia alifungiwa Mechi 8 kwa kumkashifu Kibaguzi Beki wa Manchester United Patrice Evra Mwaka 2011, aliongeza: “Ni wajibu kuishukuru Klabu, na Mashabiki wa Liverpool. Lakini kwa jinsi ninavyotendewa na waliobaki huko England imefanya Wiki hizi zilizopita kuwa ngumu. Liverpool ni Klabu ya ajabu lakini wanajua jinsi ninavyotendewa na Vyombo vya Habari!”

Suarez alijiunga na Liverpool kutoka Ajax Mwaka 2011 kwa Dau la Pauni Milioni 22.7 na Msimu uliopita alifunga Bao 30 lakini alizikosa Mechi mbili za mwisho za Ligi alipoanza kutumikia Kifungo chake cha Mechi 10 kwa kumuuma Ivanovic.

No comments:

Post a Comment