Sunday, June 2, 2013

MECHI YA MALEJENDARI: MAN UNITED 1 REAL MADRID 2

RUUD VAN NISTELROOY ACHEZEA TIMU ZOTE 2 NA KUFUNGA!

RED_HEART_UNITED LEO huko Old Trafford ilichezwa Mechi ya Kirafiki Maalum iliyoshirikisha Manguli wa Klabu za Manchester United na Real Madrid ili kusaidia Mfuko wa Hisani wa Klabu ya Manchester United uitwao RED HEART UNITED na Real waliibuka kidedea kwa kushinda Bao 2-1. 

Kabla ya Mechi hiyo kuanza, kulikuwa na utangulizi wa Shoo Laivu ya Muziki iliyofanywa na Mastaa JLS na Amelia Lily.

Real ndio walitangulia kupata Bao lililofungwa na Morientes katika Dakika ya 40 kwa shuti la nje ya Boksi lililomshinda Kipa Edwin Van Der Sar.

Man United walisawazisha katika Dakika ya 67 baada ya Andy Cole kumtengenezea Ruud Van Nistelrooy aliefunga kwa Shuti kali.

Van Nistelrooy alianza Mechi hii kwa kuichezea Real Kipindi cha Kwanza na Kipindi cha Pili kuvaa Jezi ya Man United.

Bao la ushindi kwa Real lilifungwa na Ruben De Le Red katika Dakika ya 84 alipomhadaa Kipa Van Der Gouw alieingia kuchukua nafasi ya Edwin Van Der Sar

VIKOSI:

Man United: Van Der Sar, Martin, Irwin, Johnsen, Stam, Blackmore, Scholes, Fortune, Sharpe, Cole, Yorke

Real Madrid: Contreras, Salgado, Helguera, Pavon, Amavisca, Makelele, Hierro, Figo, Zidane, Morientes, Van Nistelrooy

No comments:

Post a Comment