Sunday, June 2, 2013

BRAZIL v ENGLAND LEO KUFUNGUA MARACANA!

OXLADE-CHAMBERLAIN KUFUATA NYAYO ZA BABA YAKE!

 BRAZIL KUTUMIA MECHI KWA MATAYARISHO KOMBE LA MABARA!
 
June 2, Saa 4 Usiku Bongo Taimu
 
Estadio Jornalista Mário Filho (Maracanã)
 
Rio de Janeiro

Brazil
 
BRAZIL_SOCCER_FANS BAADA kunusurika kufutwa, Mechi ya Timu za Taifa za Brazil na England itachezwa leo Usiku huko Mjini Rio De Janeiro kwenye Uwanja wa Maracana, ambao Jina lake rasmi ni Estadio Jornalista Mário Filho, ikiwa ni ufunguzi rasmi wa Uwanja huo uliofanyiwa ukarabati mkubwa.
 
Juzi, Jaji mmoja aliamua Mechi hiyo isichezwe baada ya Uwanja huo kutotimiza masharti ya usalama lakini baadae uamuzi huo ukafutwa baada ya Rufaa.

Tangu ufanyiwe ukarabati tayari Mechi moja ya maonyesho imeshachezwa iliyowahusisha Mastaa wa zamani wakati Manguli wa Brazil, Ronaldo na Bebeto, walipoongoza Timu tofauti hapo Aprili 27 na kushuhudiwa na Watazamaji Elfu 25.

Maracana, ambayo iliwahi kupakia Watazamaji hadi 200,000, ilijengwa kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 1950 ambayo Wenyeji Brazil walifungwa kwenye Fainali yake Bao 2-1 na Uruguay waliotwaa Ubingwa wa Dunia.

Kwa mara nyingine tena, Maracana itachezwa Fainali ya Kombe la Dunia hapo Mwaka 2014 wakati Brazil watakapokuwa Wenyeji na Uwanja huo utachukua Washabiki 78,838 wote wakiwa wamekaa Vitini.


MECHI ZA BRAZIL v ENGLAND UWANJA wa MARACANA:

Brazil na England zilikutana mara ya kwanza Uwanja wa Wembley Mwaka 1956.

Mechi 11 zilichezwa Uwanja wa Wembley na nyingine huko Gothenburg, Vina Del Mar, Guadalajara, Los Angeles, Washington, Paris, Shizuoka na Doha.

Zifuatazo ni Mechi zao 5 walizocheza Maracana:

-Mei 13 1959 - Brazil 2 England 0 - Watazamaji: 200,000

-Mei 30 1964 - Brazil 5 England 1 - Watazamaji: 110,000

-Juni 12 1969 - Brazil 2 England 1 - Watazamaji: 125,000

-Juni 8 1977 - Brazil 0 England 0 - Watazamaji: 77,000

-Juni 10 1984 - Brazil 0 England 2 – Watzamaji: 56,126

JUMLA: Brazil 11 England 4 Sare 9


Mara ya mwisho kwa England kucheza Maracana ilikuwa ni Mwaka 1984 walipocheza Mechi ya Kirafiki na kuifunga Brazil Bao 2-0.

Katika Mechi hiyo, mmoja wa Wachezaji alikuwa ni Mark Chamberlain, Baba Mzazi wa Mchezaji wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain, ambae leo anatarajiwa kuichezea England na kufuata nyayo za Baba yake.

Hivi Juzi, England, ilicheza Uwanjani Wembley na kutoka sare 1-1 na Republic of Ireland na kupondwa na wengi lakini Meneja wao, Roy Hodgson, ameponda msimamo huo na kudai Timu yake ipo kwenye hali nzuri.

Nao, Brazil, chini ya Meneja Luiz Felipe Scolari, wataitumia Mechi hii kama ya kupasha moto ushiriki wao kwenye Mashindano ya FIFA, Kombe la Mabara, yatakayochezwa Nchini Brazil kuanzia Juni 15 hadi 30.

VIKOSI VINATARAJIWA:

BRAZIL:

Cesar
Alves, Thiago Silva, David Luiz, Marcelo
Fernando, Paulinho
Neymar, Oscar, Moura
Fred

ENGLAND:

Hart
Johnson, Cahill Jagielka, Cole
Carrick, Milner
Oxlade-Camberlain, Lampard, Walcott
Rooney

Refa: W. Roldán‎

No comments:

Post a Comment