Sunday, June 2, 2013

LA LIGA: MOURINHO AAGA KWA USHINDI, SOCIEDAD YATINGA ULAYA, DEPORTIVO YASHUSHWA!

BARCA_HAMASA

Real Sociedad wameipiku Valencia na kutwaa nafasi ya mwisho ya Spain kucheza UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Msimu ujao walipocheza ugenini na kuifunga Bao 1-0 Deportivo La Coruna kipigo kilichowashusha Daraja huku Jose Mourinho akiaga kwa Timu yake Real Madrid kuifunga Osasuna Bao 4-2 Uwanjani Santiago Bernabeu.
 
Valencia, walikuwa Pointi 2 mbele ya Real Sociedad kabla Mechi za mwisho za La Liga kuchezwa hiyo jana, lakini wakaambua kipigo cha 4-3 toka kwa Sevilla na ushindi wa Sociedad umewatupa nje ya UCL, Valencia.

Timu nyingine zitakazoiwakilisha Spain kwenye UCL Msimu ujao ni Mabingwa FC Barcelona, Timu ya Pili, Real Madrid, na Atletico Madrid iliyomaliza nafasi ya 3.

LA LIGA-MECHI ZA MWISHO ZA MSIMU

MATOKEO:

Real Madrid CF 4 Osasuna 2

FC Barcelona 4 Malaga CF 1 

Celta de Vigo 1 RCD Espanyol 0

Deportivo La Coruna 0 Real Sociedad 1

Real Mallorca 4 Real Valladolid 2

Rayo Vallecano 2 Athletic de Bilbao 2

Sevilla FC 4 Valencia 3

Real Zaragoza 1 Atletico de Madrid 3

Levante 1 Real Betis 1

Granada CF 2 Getafe CF 0



Bao la ushindi kwa Real Sociedad lilifungwa na Antoine Griezmann katika Dakika ya 22 na walimudu kulilinda hata pale walipokuwa Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Markel Bergara alipotolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 84.

Hii ni mara ya kwanza tangu Mwaka 2003 kwa Real Sociedad kumaliza ndani ya 4 Bora.

Sasa Valencia, kwa kumaliza Nafasi ya 5, watacheza EUROPA LIGI Msimu ujao.

Katika vita ya kushuka Daraja iliyokuwa ikizikabili Timu 4, Real Zaragoza na Real Mallorca ziliungana na Deportivo La Coruna kushuka Daraja na Celta Vigo kunusurika baada ya kuifunga Espanyol Bao 1-0 kwa Bao la Natxo Insa.

Huko Santiago Bernabeu, katika Mechi iliyoanza mapema kupita zote, Real Madrid walimuaga Meneja wao Jose Mourinho kwa kuifunga Osasuna Bao 4-2.

Mourinho anaondoka Real baada ya kukaa hapo kwa Miaka mitatu.

Bao za Real Madrid zilifungwa na Gonzalo Higuain, Dakika ya 35, Michael Essien, 38, Karim Benzema, 69, na Jose Maria Callejon, 87.

Bao za Osasuna zilifungwa na Morales Roberto Torres, Dakika ya 52 na Alvaro Cejudo, 63.

Nao Mabingwa Barcelona waliifunga Malaga Bao 4-1 kwa Bao za David Villa, Francesc Fabregas, Martin Montoya na Andres Iniesta.

MSIMAMO:

**BINGWA: Barcelona


NA
TIMU

P
W
D
L
F
A
GD
PTS

1

FC Barcelona
38
32
4
2
115
40
75
100
2

Real Madrid CF
38
26
7
5
103
42
61
85
3

Atletico Madrid
38
23
7
8
65
31
34
76
4

Real Sociedad
38
18
12
8
70
49
21
66
5

Valencia
38
19
8
11
67
54
13
65
6

Malaga CF
38
16
9
13
53
50
3
57
7

Real Betis
38
16
8
14
57
56
1
56
8

Rayo Vallecano
38
16
5
17
50
66
-16
53
9

Sevilla FC
38
14
8
16
58
54
4
50
10

Getafe CF
38
13
8
17
43
57
-14
47
11

Levante
38
12
10
16
40
57
-17
46
12

Athletic Bilbao
38
12
9
17
44
65
-21
45
13

RCD Espanyol
38
11
11
16
43
52
-9
44
14

Real Valladolid
38
11
10
17
49
58
-9
43
15

Granada CF
38
11
9
18
37
54
-17
42
16

Osasuna
38
10
9
19
33
50
-17
39
17

Celta de Vigo
38
10
7
21
37
52
-15
37
18

Real Mallorca
38
9
9
20
43
72
-29
36
19

Deportivo
38
8
11
19
47
70
-23
35
20

Real Zaragoza
38
9
7
22
37
62
-25
34

**KUSHUKA DARAJA: Real Mallorca, Deportivo La Coruna & Real Zaragoza.

No comments:

Post a Comment