Saturday, September 1, 2012

Fergie: Evra ajiandae kuwania namba

LONDON, England
ALEX Ferguson amemtaja beki Patrice Evra kama 'Askari wa Kweli' anayecheza kwa kujituma na mwenye moyo wa ushindi.

Ferguson amesema hayo wakati akimkaribisha beki mpya, Alexander Buttner ambaye ataziba pengo la Evra.

Evra, Mfaransa aliyecheza Man United mfululizo kwa miaka sita, atakabiliwa na wakati mgumu wa kuwania namba na Buttner aliyetua Old Traffor kwa ada ya uhamisho ya paundi 4 milioni.

Bosi wa United alisema: “Lazima tujipange kwa ajili ya baadaye. Evra ana miaka 31 na Alex amekuja pia kucheza nafasi ya Evra.

“Lakini hakuna aliyecheza mechi nyingi kuliko Evra katika kipindi cha miaka sita iliyopita. Amecheza akiwa majeruhi...ni mtu wa kujituma.

“Amepita kwenye mechi kwa miaka mitano. Sasa ni mechi 240 ameshacheza. Patrice amekuwa askari shujaa.

Evra amecheza mechi 291 katika kipindi cha miaka sita tangu alipojiunga kwa ada ya uhamisho paundi 5.5 milioni kutoka klabu ya Monaco.

Lakini sasa Fergie yuko tayari kufanya marekebisho kwenye kikosi chake kwa kumchezesha mlinzi Buttner raia wa Ufaransa.

Buttner (23) awasili kutoka Vitesse Arnhem na anaungana na Shinji Kagawa, Nick Powell, Angelo Henriquez na Robin van Persie kukamilisha usajili wa kipindi cha majira ya joto.

Ferguson aliongeza: “Tumekuwa tukimfuatilia Alex kwa muda sasa, anacheza kwa nguvu, anapanda kushambulia na kurudi haraka kulinda.

No comments:

Post a Comment