Tuesday, June 4, 2013

EVERTON KULIPIA KUMCHUKUA MARTINEZ, JESUS NAVAZ YUKO CITY!

JOSE MOURINHO: “KURUDI TENA CHELSEA NI UAMUZI RAHISI!”
 
SOMA ZAIDI:
WIGAN_1_CITY_0EVERTON KULIPA FIDIA YA KUMCHUKUA  MARTINEZ KWA WIGAN

Everton wamefikia makubaliano na Wigan ya kuwalipa fidia ikiwa watamchukua Meneja wao Roberto Martinez.
Martinez, Raia wa Spain mwenye Miaka 39, anatarajiwa kumbadili David Moyes ambae anahamia Manchester United kuchukua nafasi ya Sir Alex Ferguson aliestaafu.

Kuondoka kwa Martinez toka Wigan alikodumu kwa Miaka minne kulithibitishwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Dave Whelan ambae pia alisema yeye na mwenzake wa Everton walishakubaliana kuhusu Martinez.


WASIFU: Roberto Martinez

MIAKA: 39

UCHEZAJI: Real Zaragoza (1993-94), Balaguer (1994-95), Wigan Athletic (1995-2001), Motherwell (2001-02), Walsall (2002-03), Swansea (2003-06), Chester City (2006-07).

MATAJI KAMA MCHEZAJI: Copa del Rey (1994), Football League Third Division (1997), Football League Trophy (1999 & 2006)

UMENEJA: Swansea (2007-09) na Wigan Athletic (2009-13).

MATAJI KAMA MENEJA: Football League One (2008) & FA Cup (2013).

 Inatarajiwa kuhamia kwa Martinez kwenda Everton kunaweza kuthibitishwa katika Masaa 48 yajayo.
Msimu huu Martinez aliiwezesha Wigan kutwaa Kombe la FA CUP walipoifunga Manchester City Bao 1-0 lakini Siku chache baadae wakaporomoka Daraja toka BPL, Barclays Premier League na Msimu ujao watacheza Daraja la chini, Championship.

MAN CITY YAMCHUKUA WINGA WA SEVILLA JESUS NAVAS

Manchester City wamefikia makubaliano na Klabu ya Spain Sevilla ya kumnunua Winga wa Kimataifa wa Spain Jesus Navas.

Navas, mwenye Miaka 27, anategemewa kununuliwa kwa gharama ya Pauni Milioni 17.
Navas yumo kwenye Kikosi cha Spain kitakachocheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara huko Brazil kuanzia Juni 15.

Hadi sasa Man City haijatangaza nani Meneja wao mpya baada ya kumtimua Roberto Mancini ingawa wengi wanategemea Manuel Pellegrini, aliekuwa Malaga, ndio atachukua nafasi hiyo.

JOSE MOURINHO: “KURUDI TENA CHELSEA NI UAMUZI RAHISI!” 

Mara baada ya Chelsea kuthibitisha kuwa Jose Mourinho ndie atakuwa Meneja wao mpya, hii ikiwa ni mara ya pili kwa yeye kushika wadhifa huo baada ya kuwa hapo kati ya Miaka 2004 hadi 2007, Mourinho ametamka kuwa uamuzi wa kurudi kwake ulikuwa rahisi.

Mourinho alisema: “Nilimuuliza Bosi [Abramovich] unataka nirudi? Na yeye akaniuliza, unataka kurudi? Baada ya Dakika chache uamuzi ukafanywa!”

Akigusia mipango yake na Chelsea, Mourinho aligusia kuwa nia yake ni kuiboresha Timu lakini si kwa kutumia Mamilioni kuwanunua Wachezaji wapya.

Msimu huu uliopita Chelsea ilimaliza BPL ikiwa Nafasi ya 3 na pia kutwaa Kombe la EUROPA LIGI.

No comments:

Post a Comment